MSUMBIJI

Maswali yaibuka kuhusu uingiliaji wa kijeshi wa SADC nchini Msumbiji

Maelfu ya watu walitoroka mji wa Palma baada ya shambulio la wanajihadi mwishoni mwa mwezi Machi. Wengi wamepata hifadhi katika mji wa Pemba, katika mkoa wa Cabo Delgado.
Maelfu ya watu walitoroka mji wa Palma baada ya shambulio la wanajihadi mwishoni mwa mwezi Machi. Wengi wamepata hifadhi katika mji wa Pemba, katika mkoa wa Cabo Delgado. AFP - ALFREDO ZUNIGA

Kutuma mara moja wanajeshi 3,000 kaskazini mwa Msumbiji kupambana na magaidi ni moja wapo ya hatua zilizotajwa katika ripoti iliyovuja ambayo inatarajiwa kujadiliwa katika mkutano dharura wa SADC, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC, uliopangwa kufanyika Aprili 28-29.

Matangazo ya kibiashara

Jibu la kijeshi la jumuiya hiyo baada ya shambulio la wanajihadi katika mji wa Palma mwishoni mwa mwezi Machi katika mkoa wa Cabo Delgado ndio njia pekee ya kuwatimua wanajihadi hao kulingana na ripoti hiyo.

 

Tangu wakati huo, hali ya usalama bado inadorora. Ujumbe wa uchunguzi unaopendekeza kupelekwa kwa jeshi unaohofia kutokea tena kwa mashambulio baada ya mwezi wa Ramadhani

Wanataka kwenda haraka na kupeleka wanajeshi kila mahali. Wataalam wa jeshi katika ukanda huo wanapendekeza udhibiti wa anga kwa msaada wa helikopta kadhaa za kivita, ukaguzi kwenye wa baharini kwa msaawa meli na manowari, na uwepo wa wanajeshi wa nchi kavu na karibu wanajesi maalum zaidi ya 100 kwenye uwanja wa vita.

Kwa jumla, karibu askari 3,000 wanatakiwa kupelekwa nchini Msumbiji. Mpango wao umeelezewa kama ifuatavyo: kuanzishwa kwa makao makuu, kusini kabisa, katika mji wa bandari wa Nacala. Kisha kuelekea kaskazini na maeneo ya mapigano ili kushida adui.

Lengo: kudhibiti tena mji wa bandari wa Mocimboa a Praia, ambao umishikiliwa tangu mwezi Agosti 2020. Mapendekezo haya ni kutoka kwa ujumbe wa tathmini uliowekwa wakati wa mkutano wa mwisho wa SADC mapema mwezi Aprili.