CHAD

Marais Macron na Tshisekedi watoa wito kwa mabadiliko ya amani Chad

Chad, Ndjamena Aprili 27: Chad ilikumbwa na maandamano yenye vurugu katika mji mkuu na kusini mwa nchi. Angalau watu watano waliuawa.
Chad, Ndjamena Aprili 27: Chad ilikumbwa na maandamano yenye vurugu katika mji mkuu na kusini mwa nchi. Angalau watu watano waliuawa. AP - Sunday Alamba

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix-Antoine Tshisekedi, wamelaani ukandamizaji dhidi ya maandamano na vurugu vilivyotokea Jumanne hii nchini Chad.

Matangazo ya kibiashara

Felix Tshisekedi, anayeshikilia kwa sasa uongozi wa Umoja wa Afrika(AU), alipokelewa Jumatatu wiki hii katika Ikulu ya Elysée kwa chakula cha mchana na kujadili kuhusu hali inayojiri Chad. Wkati huo huo rais Emmanuel Macron ameonesha msimamo wake pale alisema kuwa anaunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia na amani wakati Ufaransa ililengwa jana katika maneneo yaliyokuwa yakitolewa jana na waaandamanaji katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena.

Katika tamko la pamoja, marais wa Ufaransa na DRC wamelaani vikali ukandamizaji dhidi ya maandamano na kutoa wito kwa Baraza la Jeshi la Mpito kuheshimu ahadi zake, hasa ile ya mabadiliko ya amani na umoja.

Siku nne baada ya ziara yake mjini Ndjamena, Emmanuel Macron pia ametaka Baraza la Kijeshi la Mpito kuwajibika.

Paris, Aprili 27: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimpokea Rais wa DRC, Félix Tsheskedi, ambaye anashikilia kwasasa uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), kwa chakula cha mchana na kuijdaili Chad.
Paris, Aprili 27: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimpokea Rais wa DRC, Félix Tsheskedi, ambaye anashikilia kwasasa uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), kwa chakula cha mchana na kuijdaili Chad. AP - Thibault Camus
Nimetoa msaada wangu kwa utulivu na uadilifu nchini Chad. Mimi nina unga mkono mabadiliko ya amani, ya kidemokrasia, yanayojumuisha wote katika uongozi wa nchi bila kubagua; Siko kwa mpango wa kutetea masuala ya kurithi. Na Ufaransa haitakuwa kamwe pamoja na wale wanaounda au kuandaa mradi huu.

"Tunataka heshima kwa ahadi zilizotolewa na Baraza la Jeshi la Mpito", ameongeza rais wa Ufaransa.