CHAD

Chad: Ujumbe wa Umoja wa Afrika ziarani Ndjamena kuendeleza mazungumzo

Polisi wa Chad wakipida doria katika mitaa ya mji wa Ndjamena wakati wa maandamano mnamo Aprili 27, 2021.
Polisi wa Chad wakipida doria katika mitaa ya mji wa Ndjamena wakati wa maandamano mnamo Aprili 27, 2021. AFP - ISSOUF SANOGO

Ujumbe wa upatanishi wa Umoja wa Afrika unatarajiwa Alhamisi hii katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena. Ujumbe huo unaoongozwa na viongozi wawili mashuhuri.

Matangazo ya kibiashara

Wanaoengoza ujumbe huu ni Bankole Adeoye, Kamishna mpya wa Amani na Usalama, na Mohamed Idriss Farah, Balozi wa Djibouti, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika. Wote wataongoza ujumbe wa wanachama kadhaa wa kamati ya amani na usalama kwa lengo la kuendeleza mazungumzo kati ya baraza la kijeshi la mpito na vyamba mbalimbali vya kisiasa.

Kulingana na chanzo cha kidiplomasia, ujumbe huo utataka kupata dhamana, kwa nafasi na mamlaka waliopewa raia, na kwa heshima ya mfumo wa kuanzia, ambapo ni kipindi cha mpito cha miezi 18. Ujumbe huu, ambao unatarajia kukutana na wadau wote kwa kipndi cha siku kumi, utatoa ripoti yake, utakapo kamilisha kazi yake. Ujumbe huu utatoa mwanga kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kupitisha msimamo wa mwisho juu ya hatua zinazoweza kuchukuliwa, kwa sababu suala hili limekuwa likisababisha mvutano mkali wa ndani kwa siku nane.

Lengo: kupunguza shinikizo la ndani katika Umoja wa Afrika

Nchi za kusini mwa Afrika, au nyingine kama Ghana, zinataka Cahd isimamishwe kwenye Umoja wa Afrika kwa sababu ya Baraza la Jeshi la Mpito kuchukua madaraka. kwa upande wa nchi hizi kilichofanywa na baraza hilo ni mapinduzi ya kijeshi, kwa sababu Katiba haikuzingatiwa. Hakuna vikwazo vyovyote vilivyochukuliwa dhidi ya Chad, nchi nyingi zilipinga, wakati tume ya Umoja wa Afrika inaongozwa na raia wa Chad, Moussa Faki Mahamat, ambaye kwa muda mrefu alikuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Idriss Déby.