CHAD

Chad: Jeshi lazindua mashambulizi katika mkoa wa Kanem

Vikosi vya usalama wakipiga doria katika mji mkuu wa Chad N'Djamena kufuatia kifo cha urais Idriss Deby aliyeuawa katika uwanja wa vita alipokuwa akiongoza mapigano na waasi, Chad Aprili 26, 2021.
Vikosi vya usalama wakipiga doria katika mji mkuu wa Chad N'Djamena kufuatia kifo cha urais Idriss Deby aliyeuawa katika uwanja wa vita alipokuwa akiongoza mapigano na waasi, Chad Aprili 26, 2021. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA

Mapigano yanaendelea katika mkoa wa Kanem kati ya jeshi na waasi kutoka kundi la Front for Alternation and Concord in Chad (FACT), kulingana na vyanzo vya jeshi.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi Aprili 29, waasi walidai kuwa wameingia katika mji wa Nokou, karibu kilomita 50 kutoka ngome za jeshi la Chad. Wanajeshi walizindua mashambulizi hayo Alhamisi jioni.

Kulingana na vyanzo vya kijeshi, mapigano yameendelea asubuhi ya leo Ijumaa, Aprili 30, katika eneo la Nokou, kilomita 250 kutoka mji mkuu, kati ya Jeshi la Mpito la Kitaifa (ANT) na waasi wa FACT. Siku ya Alhamisi, waasi walidai kuingia katika mji huu wa Nokou. Sasa wametawanyika katika maeneo mbalimbali ya mji huo, vyanzo vya jeshi vinasema, na kuongeza kuwa waasi wamesambaratishwa na wameanza kutimiliwa katika vijiji jirani na mji huo.

Chanzo kingine cha usalama kimethibitisha kuwa kulikuwa na mapigano makali Alhamisi jioni mwendo wa saa moja usiku kati ya jeshi na waasi wa FACT katika eneo hili, na kwamba katika makabiliano hayo  ANT ilidhibiti mji wa Nokou.

Kuhusu helikopta ya jeshi iliyoripotiwa kudunguliwa na waasi katika eneo hilo siku ya Alhamisi, taarifa rasmi ya jeshi inasema ilianguka. Kulikuwa na watu watatu katika ndege hiyo, vyanzo vya kijeshi vinasema: raia mmoja wa Chad na  wawili kutoka Ukraine.