CHAD

Chad yaendelea kukumbwa na mapigano, AU yajaribu kusuluhisha

Magari ya jeshi la Chad  yakionekana barabarani, wakati wapiganaji wa kundi lawaasi wa Front for Change and Concord in Chad (FACT) walionekana wakielekea mji mkuu kulingana na Marekani, huko N'djamena, Chad Aprili 19, 2021.
Magari ya jeshi la Chad yakionekana barabarani, wakati wapiganaji wa kundi lawaasi wa Front for Change and Concord in Chad (FACT) walionekana wakielekea mji mkuu kulingana na Marekani, huko N'djamena, Chad Aprili 19, 2021. REUTERS - STRINGER

Mapigano yameendelea katika eneo la Kanem Kaskazini mwa nchi ya Chad  kati ya wanajeshi na waasi waliosababisha kifo cha aliyekuwa kiongozi wan chi hiyo Idriss Derby wiki mbili zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi linasema ndege yake moja ilianguka kwa sababu ya hitilafu lakini waasi wanadai kuwa waliiangusha.

Wakati hayo yakijiri, Ujumbe wa Umoja wa Afrika umewasili jijini Ndjamena kusaidia kuanzisha mazungumzo kati ya uongozi wa kijeshi na wanasiasa.

Wanaoengoza ujumbe huu ni Bankole Adeoye, Kamishna mpya wa Amani na Usalama, na Mohamed Idriss Farah, Balozi wa Djibouti, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika. Wote wataongoza ujumbe wa wanachama kadhaa wa kamati ya amani na usalama kwa lengo la kuendeleza mazungumzo kati ya baraza la kijeshi la mpito na vyamba mbalimbali vya kisiasa.

Kulingana na chanzo cha kidiplomasia, ujumbe huo utataka kupata dhamana, kwa nafasi na mamlaka waliopewa raia, na kwa heshima ya mfumo wa kuanzia, ambapo ni kipindi cha mpito cha miezi 18. Ujumbe huu, ambao unatarajia kukutana na wadau wote kwa kipndi cha siku kumi, utatoa ripoti yake, utakapo kamilisha kazi yake. Ujumbe huu utatoa mwanga kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika