DRC-USALAMA

DRC: Jean Michel Sama Lukonde aahidi kurejesha usalama Lubumbashi

Sama Lukonde Kyenge aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rais Félix Tshisekedi Februari 15, 2021.
Sama Lukonde Kyenge aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rais Félix Tshisekedi Februari 15, 2021. © Capture d'écran chaîne Youtube Sama Lukonde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kiidemokrasia ya Congo amehitimisha ziara yake huko Lubumbashi, katika mkoa wa Katanga, alikozaliwa. Ziara yake haikuwa ya kiserikali lakini ilikuwa rasmi.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Sama Lukonde katika mji wa Lubumbashi haikuwa ya kiserikali lakini ilikuwa na lengo kubwa, kwanza ni mzaliwa wa Katanga, alikwenda kutoa heshima zake kwa kiongozi mwingine wa mkoa huo, Lukonde Kyenge, ambaye ni baba yake.

Lukonde Kyenge alikuwa mwanzilishi mwenza wa chama cha UFERI, na aliuawa mwezi Aprili 2001, karibu kilomita kumi kutoka mji wa Lubumbashi, wakati wa utawala wa Joseph Kabila alikuwa akiomba mazungumzo yatakayowajumuisha wadau wote kwa ujenzi wa taifa.

Ziara hii mjini Lubumbashi pia ilikuwa rasmi. Jean Michel Sama Lukonde alijikita kuhusu hali ya usalama katika mkoa wa Katanga. Alipowasili tu mada kuu ilihusu suala la usalama katika mkoa huo. Waziri Mkuu alikumbusha ahadi yake katika vita dhidi ya uhalifu wa mijini huko Lubumbashi ambapo, kila jioni, familia zinashambuliwa na majambazi wenye silaha ambao huiba, kuua na kubaka. Vikosi vya usalama mara nyingi wanatuhumiwa kuhusika katika vitendo hivi vya uhalifu.

Lubumashi haikuchukuliwa hatua mikoa ya Kivu Kusini na Ituri

"Kazi yetu ya kwanza ni kurejesha amani," alisema Waziri Mkuu, huku akiongeza: “Tumechoka na ukosefu wa usalama tunaoujua nchini. "

Maneno haya aliyasema Jumamosi hii wakati wa baraza la mawaziri katika mkoa wa Katanga. Lakini hapa, hakutanga hali ya hatari kama ilivyoamuliwa kwa mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, ambayo pia ni inakabiliwa na ukosefu wa usalama.

Waziri mkuu wa DRC amesema ametoa maagizo kwa wanajeshi na maafisa wa polisi kumaliza tatizo hilo la ukosefu wa usalama. hata hivyo hakutoa maelezo zaidi.