CHAD

Chad: Baraza la Jeshi launda serikali yake ya mpito

Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno Aprili 11, 2021 huko Ndjamena.
Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno Aprili 11, 2021 huko Ndjamena. © MARCO LONGARI/AFP

Baraza la Kijeshi (CMT) lililokuwa madarakani nchini Chad tangu kifo cha rais Idriss Déby Itno limetangaza serikali yake ya mpito, msemaji wa jeshi ametangaza kwenye runinga ya serikali. Baraza hilo pia ilmetangaza kufuta sheria ya kutotoka nje.

Matangazo ya kibiashara

Mahamat Idriss Déby, mtoto wa hayati rais Idriss Deby Itno, ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa Baraza la Jeshi la Mpito (CMT),  ameteua kwa agizo la kirais mawaziri 40 na maafisa waandamizi wa serikali, na kuunda Wizara mpya ya Maradhiano ya Kitaifa.

Acheikh ibn Oumar ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya Maridhiano na Mazungumzo. Acheikh ibn Oumar, kiongozi wa zamani wa kivita, waziri wa zamani wa Hissène Habré, aliyerejea nchini Chad mwaka 2018 baada ya miaka 25 ya kuwa uhamishoni na kuwa mshauri wa Idriss Déby.

Kwenye wizara ya mambo ya nje ameteuliwa Chérif Mahamat Zène, aliyekuwa mshirika wa karibu wa Idriss Déby ambaye aliwahi kushikilia wadhifa huo, na kuwa katibu mkuu na msemaji wa chama cha MPS.

Maafisa wawili wakuu wameteuliwa: Jenerali Daoud Yaya Brahim anakuwa Waziri Mjumbe anayehusika na masuala ya ulinzi kwenye ikulu ya kiongozi wa baraza la Kijeshi. Wizara ambayo alikuwa tayari ameshikilia chini ya utawa wa Idriss Déby; Jenerali Souleyman Abakar Adoum, mmoja wa wajumbe kumi na tano wa Baraza la Jeshi la Mpito, ameteuliwa kuwa Waziri wa Usalama wa Umma.

Lydie Beassemda, ambaye alikuwa mgombea wa chama cha PDI katika uchaguzi wa urais mwezi uliopita, sasa ni waziri wa elimu ya juu. Issa Doubragne, ambaye tayari alikuwa Waziri wa Uchumi, anaendelea kushikilia wizara hiyo. Patalet Geo, rafiki wa karibu wa Waziri Mkuu Albert Pahimi Padacké, anachukua Wizara ya Miundombinu. Fatima Goukouni Weddeye ameteuliwa kuwa waziri wa Uchukuzi, hadi sasa alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la uwekezaji . Kosmadji Merci anakuwa Waziri wa Elimu. Alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanaunda timu ya kampeni ya Idriss Deby katika uchaguzi wa urais uliopita.