DRC

DRC: Kesi ya Jenerali Delphin Kahimbi kufunguliwa Jumatatu

Delphin Kahimbi, alikuwa amesimamishwa kazi siku mbili kabla ya kifo chake, baada ya kukamatwa Februari 20, 2020 na idara ya uhamiaji (DGM), wakati alikuwa kakijianda kusafiri kwenda Afrika Kusini.
Delphin Kahimbi, alikuwa amesimamishwa kazi siku mbili kabla ya kifo chake, baada ya kukamatwa Februari 20, 2020 na idara ya uhamiaji (DGM), wakati alikuwa kakijianda kusafiri kwenda Afrika Kusini. AFP PHOTO / Walter ASTRADA

Kesi ya mauaji ya Jenerali Delphin Kahimbi, naibu mkuu wa zamani wa jeshi la FARDC, aliyepatikana amefariki dunia nyumbani kwake Februari 28, 2020 huko Kinshasa, inafunguliwa Jumatatu hii Mei 3 huko Kinshasa, nchini DRC.

Matangazo ya kibiashara

Watu sita akiwemo mjane wa jenerali huyo, Brenda Nkoy, watafikishwa katika mahakama ya Kinshasa-Gombe kusikilizwa. Wanatuhumiwa kwa mauaji ya kukusudia na kushiriki katika tume ya mauaji.

Meja Jenerali Delphin Kahimbi alifariki dunia Februari 28, 2020 huko Kinshasa.

Alikuwa amesimamishwa kazi siku mbili kabla ya kifo chake, baada ya kukamatwa Februari 20, 2020 na idara ya uhamiaji (DGM), wakati alikuwa kakijianda kusafiri kwenda Afrika Kusini.

Jenerali Delphin Kahimbi, aliyedaiwa kuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani Joseph Kabila, alishikilia wadhifa wa Naibu mkuu wa jeshi la FARDC kwa miaka sita. Kabla ya hapo, alisimamia operesheni za Kimya 2 katika mkoa wa Kivu Kusini na naibu mkuu anayesimamia operesheni na ujasusi kwa kanda ya 34 ya jeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Uchunguzi wa jeshi

Makao makuu ya jeshi ilithibitisha, katika tangazo lililotiwa saini Februari 28, 2020 na Mkuu wa jeshi la FARDC, Jenerali Célestin Mbala kwamba hatua zote zimezingatiwa kubainisha mazingira ya kifo cha Jenerali Delphin Kahimbi.