NIGER-USALAMA

Niger: Wanajeshi 15 wauawa katika shambulio katika mkoa wa Tahoua

Mohamed Bazoum akizuru kambi ya jeshi huko Bosso, mkoa wa Diffa akiambatana na wanajeshi.
Mohamed Bazoum akizuru kambi ya jeshi huko Bosso, mkoa wa Diffa akiambatana na wanajeshi. © AFP - Issouf Sanogo

Kulingana na vyanzo vya usalama, angalau wanajeshi kumi na tano waliuawa Jumamosi Mei 1 katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha katika eneo la Tahoua, kilomita 500 kaskazini mashariki mwa Niamey.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na katika eneo hilo, karibu saa 2 usiku, doria ya vikosi vya ulinzi na usalama ilishambuliwa karibu na mji wa Agando walipokuwa wakifuata watu waliokuwa kwenye pikipiki.

Mapigano mkali yalitokea. Hasara kwa upande wa washambuliaji bado haijulikani. Watu hao wenye silaha waliweza kuondoka na magari mawili ya jeshi la Niger.

Hata hivyo, "watu ishirini na wanne wanaoshukiwa kuwa magaidi" waliokamatwa siku ya Jumatano na jeshi katika mkoa wa Tillabéril, magharibi mwa Niger karibu na Mali, waliuawa wakati wakijaribu kutoroka, taarifa ya serikali imesema.

Shambulio la doria ya jeshi lilifanyika Jumamosi alasiri katika mkoa wa Tahoua, katika eneo ambalo mashambulio yalisababisha vifo vya watu 137 mwezi Machi mwaka huu.

Chanzo cha shambulio hilo hakijabainika lakini akundi kadhaa ya wanajihadi yenye mafungmano na Al Qaeda au ISIS yako katika mkoa huo.

Makundi haya, mara nyingi kutoka Mali, yamewaua wanajeshi mia kadhaa wa Niger  tangu mwaka 2018