AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini: Vita vya urithi vyaibuka kwa ufalme wa Zulu

Mfalme wa Zulu Goodwill Zwelithin (katikati) hapa ilikuwa mwezi wa Septemba 2019 na kiongozi wa chama cha Inkatha Mangosuthu Buthelezi (kulia), alikufa mwezi wa Machi 2021 baada ya miaka hamsini ya utawala. Mzozoumeibuka ndani ya familia ya kifalme ya Zulu kuhusu nani atakaye chukuwa mikoba yake.
Mfalme wa Zulu Goodwill Zwelithin (katikati) hapa ilikuwa mwezi wa Septemba 2019 na kiongozi wa chama cha Inkatha Mangosuthu Buthelezi (kulia), alikufa mwezi wa Machi 2021 baada ya miaka hamsini ya utawala. Mzozoumeibuka ndani ya familia ya kifalme ya Zulu kuhusu nani atakaye chukuwa mikoba yake. AFP - RAJESH JANTILAL

Tangu kifo cha Mfalme Goodwill Zwelithini mwezi Machi mwaka huu, mmoja wa wajane wake alikuwa ameshikilia nafasi hiyo hadi uteuzi wa mfalme mpya. Lakini pia alifariki wiki iliyopita, akiwa na umri wa miaka 65, na atazikwa Alhamisi alfajiri, kulingana na mila za kifalme. Kifo ambacho kimezidi kudhoofisha umoja ndani ya ukoo wa kifalme, na kuibua mvutano katika familiaya kifalme.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yanaendelea kuongezeka katika kasri ya kifalme ya Nongoma, katika mkoa wa KwaZulu-Natal, wakati mazishi ya Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini Zulu, aliyefariki mwishoni mwa mwezi Aprili, yakikaribia. Wakati familia ya kifalme hadi sasa ilikuwa imeonyesha picha ya umoja, na kushauriana kwa faragha ili kujua ni nani atakayechukuwa nafasiya mfalme, sasa malumbano yameanza kujitokeza hadharani, huku baadhi ya watu wa familia ya kifalme wakifanya mikutano na waandishi wa habari na wengine wakitoa taarifa mbalimbali zinazokinzana.

Baadhi ya watu kutoka familia ya kifalme wameamua kuwasilisha malalamiko yao mahakamani ... Mke wa kwanza kati ya wake sita wa Mfalme Zwelithini anaomba mahakama kumtambua kama mke mkuu, kwani ndiye pekee aliyeolewa na mfalme kwa ndoa rasmi inayofuata sheria za nchi. Katika malalamiko mengine, binti zake wawili wanabaini kuwa wosia ulioachwa na baba yao ni ulighushiwa, na wanaomba usimamishwe.

Goodwill Zwelithini, mfalme wa Zulu tangu mwaka 1971 na ambaye alifariki mwezi Machi akiwa na umri wa miaka 72, alikuwa mfalme mwenye ushawishi mkubwa nchini Afrika Kusini, mamlaka ya maadili kwa Waafrika Kusini milioni 12. Waziri wa Mambo ya Jadi, ambaye alikuja kutoa heshima zake kwa hayati Malkia, kwa hivyo anatumai kuwa amani na utulivu vitarejea haraka ndani ya familia ya kifalme.