DRC-USALAMA

DRC: Rais Tshisekedi aagiza jeshi kusimamia usalama Ituri na Kivu Kaskazini

Rais Tshisekedi. (picha ya kumbukumbu)
Rais Tshisekedi. (picha ya kumbukumbu) ISSOUF SANOGO / AFP

Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeagiza wanajeshi na polisi kushika mamlaka zote za kiraia katika mikoa miwili ambayo imewekwa chini ya sheria ya kijeshi.

Matangazo ya kibiashara

Mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, mashariki mwa DRC ambako makundi kadhaa ya waasi yanaendesha kuhujumu raia na kupora mali zao imewekwa chini ya sheria ya kijeshi.

Serikali za mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini, na mamlaka za mikoa hiyo, itawekwa chini ya ofisi za jeshi la DR Congo au polisi ya taifa. Utekelezwaji wa mamlaka za kiraia utafanywa na mamlaka za kijeshi hadi amani itakaporejeshwa

Msemaji wake, Tharsice Kasongo Mwema amethibitisha kuwa mikoa hiyo imetangazwa kuwa chini ya sheria ya kijeshi kwa siku 30 kuanzia Alhamisi ya Mei 6.

Katika hotuba iliyorushwa na televisheni ya taifa Jumatau wiki hii, Rais Felix Tshisekedi alisema amesikia kilio cha wananchi katika mikoa hiyo inayokumbwa na machafuko na mauaji ya kikatili.