NIGERIA-USALAMA

Kumi wauawa katika shambulio kaskazini mwa Nigeria

Raia wengi wameyatoroka makazi yao kufuatia mashambulizi ya makundiyenye silaha katika mkoa wa Borno, Nigeria.
Raia wengi wameyatoroka makazi yao kufuatia mashambulizi ya makundiyenye silaha katika mkoa wa Borno, Nigeria. AP - Sunday Alamba

Zaidi ya watu kumi,ikiwa ni pamoja na wanajeshi saba, wameuawa na wapiganaji wa Kiisilamu katika shambulio huko kaskazini mashariki mwa Nigeria, kulingana na vyanzo vinne vya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji waliwasili kwa pikipiki katika eneo lenye wakazi wengi kutoka jamii ya Ajiri, katika mkoa wa Borno Jumapili asubuhi, ambapo waliua afisa wa jeshi na wanajeshi sita, vyanzo hivyo vimesema. Pia waliua raia sita, walichoma moto nyumba na kuchukua vitu vya thamani, vyanzo hivyo vimeongeza.

Katika taarifa, jeshi la Nigeria limesema wanajeshi wake walijaribu kuzima shambulio hilo lakini waasi waliwapiga risasi wakaazi wengine na wanajeshi wawili.

Mashambulio ya aina hii yameongezeka katika mkoa huo katika miezi ya hivi karibuni, na makumi ya wanajeshi wameuawa na maelfu ya watu wameyatoroka makazi yao.