BURKINA FASO-USALAMA

Thelathini wauawa mashariki mwa Burkina Faso

Kijiji cha Kodyel, mashariki mwa Burkina Faso, kilikumbwa na shambulizi kali la kigaidi Mei 3 na kusababisha vifo vya watu kadhaa.
Kijiji cha Kodyel, mashariki mwa Burkina Faso, kilikumbwa na shambulizi kali la kigaidi Mei 3 na kusababisha vifo vya watu kadhaa. © google maps

Raia wasiopungua 30 wameuawa Jumatatu (Mei 3) katika shambulio dhidi ya  kitongoji cha kilimo cha Kodyel, katika eneo la Foutouri, karibu kilomita 145 kutoka mji wa Fada Ngourma katika mkoa wa mashariki, nchini Burkina Faso.

Matangazo ya kibiashara

Watu wasiojulikana wenye silaha walivamia kijiji hicho mapema asubuhi ya jana na kushambulia raia, licha ya watu waliojitolea kwa ulinzi wa taifa, kundi linalosaidia vikosi vya jeshi, kuingilia kati. Karibu watu 30 wameliuawa, nyumba kadhaa zilichomwa moto.

Washambuliaji walivunja kituo cha kilimo cha Kodyel karibu saa 5 asubuhi Jumatatu. Kulingana na ushuhuda uliokusanywa na vyanzo vya usalamakatika eneo hilo, waliotekeleza shambulio hilo walikuwa karibu 300 na shambulio hilo lilidumu saa mbili.

"Walizingira kijiji na kuuwa karibu wanaume wote," anaelezea shahidi aliyetajwa na chanzo chetu. Wanawake na watoto tu waliowekwa kando. Idadi kamili ya wahanga bado haijulikani kwa wakati huu. Gavana wa mkoa wa Mashariki amebaini kwamba raia wengi waliuawa. Vyanzo vya usalama vinasema watu wasiopungua 30, pamoja na watu wawaili kutoka kundi linalosaidia jeshi waliuawa katika shambulio hilo. Miongoni mwa raia waliouawa ni mkuu wa kijiji na watu kadhaa wa familia yake. Kuna watu karibu ishirini waliojeruhiwa pia. Kwa kuongezea, washambuliaji kadhaa walipigwa risasi na kuuawa na kundi linalosaidia jeshi kulinda taifa.