ETHIOPIA-SIASA

Uchaguzi Ethiopia: EU haitatuma ujumbe wa waangalizi katika uchaguzi wa Juni 5

Mkuu wa sera ya nje na usalama wa Umoja wa Ulaya,Josep Borrel.
Mkuu wa sera ya nje na usalama wa Umoja wa Ulaya,Josep Borrel. Kenzo Tribouillard Pool/AFP/Archivos

Umoja wa Ulaya umetangaza kwamba hautatuma ujumbe wa wa waangalizi wa uchaguzi wa wabunge utakaofanyika nchini Ethiopia mnamo Juni 5.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa Sera za Nje Josep Borrel amesikitishwa na kuona hawakupewa dhamana za kutosha kuhakikisha kuwa uchaguzi huo utakuwa huru.

Mwezi uliopita, Josep Borrel alionya, wakati wa kutangazwa msaada wa euro milioni 53 katika masuala ya kibinadamu kwa Ethiopia: ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya katika uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika mwezi Juni utabaki kama ilivyo, "isipokuwa, alisema, hali inazidi kuwa mbaya ".

Kubadilika kwa kauli katika taarifa yake Jumatatu wiki hii, inaonyesha kutokubaliana na Ethiopia kuhusu kutumwa kwa ujumbe huu nchini Ethiopia. Amebaini kwamba Ethiopia "imekataa kuheshimu masharti yanayotakiwa kimataifa kwa kutumwa kwa ujumbe wowote wa waangalizi wa uchaguzi", hasa kwa sababu Addis Ababa inakataa kwamba waangalizi kutoka Umoja aw Ulaya wawe na mfumo wao wa mawasiliano. Kwa upande mwingine, uamuzi wa kutoa euro milioni 20 kusaidia Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi utatekelezwa, amesema.