MSUMBIJI-USALAMA

Barabara mpya za biashara haramu zaripotiwa Cabo Delgado

Picha iliyopigwa Februari 24, 2021 inaonyesha nyumba za muda katika Kituo cha Kilimo cha Napala wilayani Metuge, Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji. Mahali panatumika kama kituo cha watu waliokimbia makazi yao waliokimbia kutokana na mashambulio ya waasi wenye silaha katika mkoa wa kaskazini wa jimbo la Cabo Delgado. Watu 3,000 wanaishi huko kwa sasa kulingana na takwimu za serikali.
Picha iliyopigwa Februari 24, 2021 inaonyesha nyumba za muda katika Kituo cha Kilimo cha Napala wilayani Metuge, Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji. Mahali panatumika kama kituo cha watu waliokimbia makazi yao waliokimbia kutokana na mashambulio ya waasi wenye silaha katika mkoa wa kaskazini wa jimbo la Cabo Delgado. Watu 3,000 wanaishi huko kwa sasa kulingana na takwimu za serikali. AFP - ALFREDO ZUNIGA

Mgogoro wa usalama katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji hauelemei tu uchumi halali, hasa juu ya kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji gesi kutoka kampuni ya Ufaransa ya TOTAL baada ya shambulio la mji wa Palma mwishoni mwa Machi.

Matangazo ya kibiashara

Mgogoro huu pia una athari kwenye mitandao ya biashara katika ukanda mzima. Katika mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji, kwenye mpaka na Tanzania, kundi la waasi wenye silaha lililoanzishwa mnamo mwaka 2017 linaendelea kujidhatiti.

Kundi hili lilitangaza kujiunga na kundi la Islamic State. Na kuongezeka kwa mzozo na vikosi vya serikali kunasababisha wafanyabiashara wa magendo kuimarisha njia zao.

Wataalam hapo awali walidhani kwamba waasi watajaribu kudhibiti njia za biashara haramu kujipatia fedha. Jimbo la Cabo Delgado kihistoria ni eneo la wapita njia na wafanya biashara wa kila aina. Kwa barabara kupitia mpaka wa Tanzania, au kwa bahari, kando ya pwani ya Uswahilini hadi Zanzibar. Lakini wakati wa uchunguzi wao  mwezi Januari na Februari, wachunguzi wa shirika la Global Initiative waliona kuwa njia za magendo zinapita katika eneo linalodhibitiwa na waasi kwa sasa.

Dawa za kulevya zinazokusudiwa kutumiwa na wenyeji hazipitii tena barabara ya mpaka wa Negomano, lakini zinapitishwa zaidi magharibi, baada ya siku mbili zaidi kwa kutumia barabara. Wakati huo, boti znazobeba dawa za kulevya aina ya Heroini na Methamphetamine kutoka afhanistani hazipitishwi tena Mocimboa da Praia, bali kilomita 700 kusini, katika mkoa wa Nampula. Vivyo hivyo kwa wahamiaji haramu wanaotumia njia ya baharini, wanaotoka Pembe ya Afrika, wanatuwa Zanzibar, kabla ya kuingia huko Cabo Delgado na kusafiri hadi Afrika Kusini kwa basi.