DRC-USALAMA

Hali ya dharura DRC: Majina ya magavana wapya wa jeshi yafichuliwa

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mei 4, 2021. Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, serikali, polisi na wasemaji wa jeshi walielezea kuhusu hatua zinazohusiana na hali ya dharurura katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mei 4, 2021. Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, serikali, polisi na wasemaji wa jeshi walielezea kuhusu hatua zinazohusiana na hali ya dharurura katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini. © Sonia Rolley / RFI

Hatimaye majina ya magavana wa kijeshi wa mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamejulikana. Wanatarajiwa kuanza kazi Alhamisi wiki, wakati hali ya dharura iliyotangazwa na Rais Felix Tshisekedi katika mikoa hiyo itaanza kutekelezwa.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, wasemaji wa serikali, jeshi na polisi walielezea na kuhakikisha kuhusu mazingira ya hali hii ya dharura ambayo wakati mwingine inatia wasiwasi raia.

Rais wa DRC ameamua kuamini viongozi wawili wa zamani wa waasi kuongoza mikoa hii miwili kwa mwezi mmoja, mikoa inayotia hofu na mauaji, ili hali wakati wa mkutano na waandishi wa habari, wasemaji wa serikali, jeshi na polisi walituliza nyonyo raia kuhusu mazingira ya hali hii ya dharura iliyotangazwa siku chache zilizopita.

Jeshi na polisi wapewa majukumu ya kuiongoza mikoa ya ITuri na Kivu Kaskazini

Gavana wa jeshi wa Kivu Kaskazini ni Jenerali Luboya Nkashama, mkuu wa zamani wa kanda ya kwanza ulinzi, ambayo inajumuisha Kinshasa kati ya mikoa mingine, pia alikuwa kamanda wa kanda ya 13 ya jeshi katika eneola Equateur. Afisa huyu, mzaliwa wa eneo la Kasai, ni kiongozi wa zamani wa waasi  wa RCD Goma, karibu na Rwanda, ambapo wakati mmoja iliongoza mkoa huu. Tayari ameshtumiwa na baadhi ya mashirika ya kiraia kwa ukatili aliufanya dhidi ya raia. Jenerali Luboya Nkashama, kama inavyotarajiwa, atasaidiwa na afisa wa polisi, Kamishna Alonga Boni Benjamin.

Huko Ituri, kiongozi wa waasi wa zamani pia ameteuliwa, lakini anatoka katika kundi la waasi la MLC la makamu wa rais wa zamani na mshirika wa karibu wa Felix Tshisekedi, Jean-Pierre Bemba anaochukuliwa kama mtu wa karibu na Uganda. Jenerali Constant Ndima Kongba alikuwa kamanda wa kanda ya tatu ya ulinzi ambayo inajumuisha Kivu mbili, Maniema na Tshopo. Hadi wakati huo alikuwa naibu mkuu wa majeshi anayehusika na masuala ya utawala na vifaa. Naibu wake gavana ni kamishna Ekuka Lipopo.