MALI

Mwanahabari wa Ufaransa ashikiliwa mateka na kundi la wanajihadi Mali

Picha ya mwandishi wa habari wa Olivier Dubois kwenye Twitter.
Picha ya mwandishi wa habari wa Olivier Dubois kwenye Twitter. © Capture d'écran

Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka, RSF, linaomba Olivier Dubois aachiliwe kuru mara moja na bila masharti. Mwanahabari huo kutoka Ufaransa alikuwa akifanyia kazi katika mkoa wa Gao, nchini Mali, wakati alitekwa nyara, linasema shirika hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mwanahabari Olivier Dubois anadai katika video kwamba alitekwa nyara Aprili 8, 2021 huko Gao, nchinj Mali, na tangu wakati huo yuko mikononi mwa GSIM, kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu, linalofungamana na Al-Qaeda. Katika video hyo, anatoa wito kwa familia yake, marafiki zake na viongozi wa Ufaransa kusaidia ili aweze kuachiliwa.

"Tuliarifiwa siku mbili baada ya kutoweka kwake," amesema Christophe Deloire kiongozi wa RSF. "Kwa kushauriana na vyombo vya ahbari ambavyo vilimuajiri, tumechukua uamuzi wa kutoweka hadharani kisa hiki cha kumteka nyara, ili tusizuie matokeo chanya ya haraka kuhusu kuachiliwa kwake."

Shirika la Waandishi Wasio na Mipaka sasa wanaomba hadharani "Mamlaka nchini Mali na Ufaransa kufanya kila wanachokiweza kusaidiwa anaachiliwa".