DRC-USALAMA

Hatua ya rais Tshisekedi yaanza kutumika katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri

Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mkoa wa Ituri (picha ya pkumbukumbu).
Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mkoa wa Ituri (picha ya pkumbukumbu). SAMIR TOUNSI / AFP

Hali ya dharura inaanza kutekelezwa Alhamisi, Mei 6 katika katika mikoa inayokumbwa na machafuko mabaya ya Kivu Kaskazini na Ituri, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Magavana wa kijeshi wameteuliwa. Kuna pia makamu wa magavana ambao ni maafisa wa polisi.

Matangazo ya kibiashara

Katika ngazi zote za utawala, vikosi vya usalama vinatakiwa kuchukua madaraka. Lengo: kurejesha amani katika mikoa hii ambayo imekumbwa na mizozo kutokana mashambulizi ya makundi yenye silaha kwa zaidi ya miaka ishirini.

Kazi ni kubwa sana. Magavana hawa wa kijeshi watalazimika sio tu kusimamia mikoa hii kwa angalau mwezi mmoja- wana makamu wa magavana na baraza la mawaziri la kuwasaidia - lakini pia watalazimika kufanya operesheni za kijeshi. Usimamizi wa kila siku, operesheni za kijeshi na usimamizi katika mahakama...

"Kuanzia Alhamisi hii, katika mikoa hii miwili, mahakama ya kijeshi inachukua nafasi ya kwanza kuliko majakama za kiraia. Rais Tshisekedi alisema ameiagiza serikali kutoa msaada unaofaa wa vifaa na kifedha. Hii ni moja ya wasiwasi wa mashirika ya kiraia. Je! Jeshi na polisi watawezaje kushughulikia kila kitu kwa wakati mmoja", Mobert Senga, mwanaharakati wa DRC na mtafiti katika shirikala kimataifa la haki za inadamu la Amnesty International, amesema

Tunaelewa umuhimu wa haraka unaotakiwa kufanywa kwa kuchukuwa hatua kumaliza mauaji katika mikoa hii. Muktadha na yaliyomo katika kurejesha usalama na amani katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri husababisha matatizo kadhaa. Je! Hatua hii ni muhimu na inaendana na hatari? Kwa kuzingatia kuwa hali ya kuzingirwa imetangazwa katika mikoa yote wakati vurugu kubwa zaidi ziko katika baadhi ya maeneo, tatizo kubwa ni nguvu na uwezo mkubwa waliopewa viongozi wa jeshi.