MALI

Morocco: Mwanamke kutoka Mali ajifungua watoto tisa, maajabu ya dunia

Nchini Morocco, mwanamke kutoka wa Mali ajifungua watoto tisa.
Nchini Morocco, mwanamke kutoka wa Mali ajifungua watoto tisa. Getty Images/ERproductions Ltd

Uzazi wa ajabu baada ya ujauzito ambao ulisababisha mtafaruku nchini Mali na kuongezeka kwa mshikamano kumsafirisha mama huyo. Halima Cissé, 25, kutoka Timbuktu, alisafirishwa kwenda Morocco mwishoni mwa mezi Machi kwa ufuatiliaji wa karibu na kupatiwa huduma sahihi na ya kutosha.

Matangazo ya kibiashara

Mwanamke huyo huyo alitarajia kupata watoto saba. Alizaa watoto tisa, kwa njia ya upasuaji, Jumanne, Mei 4.

Serikali ya mpito ya Mali ndio ambayo ilitangaza tukio hilo kwa mara ya kwanza. Habariimegonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari nchini Mali. Watoto wote tisa walizaliwa hai, ikiwa ni tukio la kwanza duniani.

Halima Cissé anahudumiwa katika kliniki ya kibinafsi ya Aïn Borja huko Casablanca. Mwishoni mwa mwezi Machi, wakati huo alikuwa na ujauzito wa miezi mitano na nusu, mapema sana kuzaa, licha ya kuumwa. Kila kitu kinafanywa ili kuokoa muda.