NIGERIA-USALAMA

Wanafunzi waliotekwa nyara waachiliwa Nigeria

Wanajeshi wa Nigeria wakiwa katika kituo cha ukaguzi mnamo 2015 (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa Nigeria wakiwa katika kituo cha ukaguzi mnamo 2015 (picha ya kumbukumbu). © Lekan Oyekanmi/AP

Wanafunzi thelathini waliotekwa nyara mwezi Machi na kundi la watu waliojihami kwa silaha za kivita kaskazini mwa Nigeria wameachiliwa, kitendo ambacho kilikaribishwa Jumatano wiki hii na rais wa Nigeria, anayekosolewa kwa kushindwa kuzuia mashambulio ya magenge ya wahalifu wanaofanya utekaji nyara wa watu wengi.

Matangazo ya kibiashara

"Tunafurahi kuwa waliachiliwa ... Tunawashukuru wahusika wote waliochangia kwa kitendo hiki cha kufurahisha", alisema Rais Muhammadu Buhari katika taarifa.

Jumla ya wanafunzi 39 waliotekwa nyara mnamo Machi 11 katika chuo kikuu cha kaskazini magharibi mwa Nigeria, katika mji wa Kaduna.

Kundi la kwanza la wanafunzi kumi lilipatikana kwa msaada wa vikosi vya usalama katika wiki zilizofuata shambulio hilo, lakini wanafunzi 29 waliokuwa wamesalia walitekwa nyara kwa karibu miezi miwili.

"Makao makuu ya polisi yaliarifu serikali ya Jimbo la Kaduna juu ya kuachiliwa kwa wanafunzi hao" waliotekwa nyara mnamo Machi 11, Samuel Aruwan, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jimbo la Kaduna, amesema.

Visa vya utekaji nyara wa watu wengi shuleni umeongezeka kaskazini na katikati mwa Nigeria, vitendo vinavyotekelezwa na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu au magenge ya wahalifu wanaojulikana katika eneo hilo kama "majambazi" wanaomba fidia au kuwa na uhusiano na makundi haya yenye silaha.