NIGER-USALAMA

Niger: Mashambulizi yaongezeka katika mikoa ya mpakani na Mali

Eneo la Tillabéry nchini Niger (picha ya kumbukumbu) ambapo shambulio la mauaji dhidi ya jeshi la Niger lilitokea, Jumatano Mei 15.
Eneo la Tillabéry nchini Niger (picha ya kumbukumbu) ambapo shambulio la mauaji dhidi ya jeshi la Niger lilitokea, Jumatano Mei 15. RFI/Sayouba Traoré

Nchini Niger, shambulio jipya liliua wanajeshi 15 na wengine wanne kujeruhiwa Jumanne, Mei 4, katika mkoa wa Tillabéry magharibi mwa nchi. Wizara ya Ulinzi ilitangaza katika taarifa kwa waandishi wa habari Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Hili ni shambulio kubwa la pili lililokumba vikosi vya jeshi vya Niger katika siku 4, na kufanya idadi ya awanajeshi waliouawa kufikia zaidi ya 31.

Shambulio hilo jipya lililenga ngome ya wanajeshi wa Niger, ambao Jumanne wiki hii. Shambulio ambalo lilitekelezwa na "watu wenye silaha za kivita" kulingana na taarifa  kutoka wizara ya ulinzi ya Niger. Wanajeshi wakati huo walikuwa katika eneo la Intoussan, karibu na mji wa Banibangou, kilomita chache kutoka mpaka wa Mali.

Jumamosi, shambulio jingine la kuvizia lililenga wanajeshi wa kikosi cha walinzi wa taifa katika mkoa wa Tahoua, kaskazini mashariki mwa nchi. Kulingana na vyanzo nchini Niger, doria ya kikosi hicho ilizigirwa na watu wenye silaha kuelekea kijiji cha Agando, wakati ilipokuwa ikifuata kundi la watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki. Wanajeshi 16 waliuawa na magari mawili yalipelekwa na magaidi hao, kulingana na vyanzo vya usalama.

Mashambulio haya yanakuja wiki chache baada ya mauaji ya yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 300 katika maeneo ya Banibangou na Tilia, mpakani na Mali.