DRC-USALAMA

DRC: Utata waendelea juu ya uteuzi wa waasi wa zamani kama magavana wa jeshi

DRC (Mei 4, 2021): Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, serikali, polisi na wasemaji wa jeshi walielezea kuhusu hali ya tahadhari iliyotangzwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri (Picha ya kumbukumbu).
DRC (Mei 4, 2021): Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, serikali, polisi na wasemaji wa jeshi walielezea kuhusu hali ya tahadhari iliyotangzwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri (Picha ya kumbukumbu). © Sonia Rolley / RFI

Magavana wapya wa kijeshi walioteuliwa hivi karibuni kuongoza mikoa iliyowekwa chini ya hali ya dharura, mashariki mwa Jamhuri ay Kidemokrasia ya Congo hawajawasili katika miko hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Tangu Alhamisi, hali ya dharura inatekelezwa vilivyo katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Lengo ni kukomesha mauaji katika mikoa hii miwili. Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch linasema lina wasiwasi kuhusu  watu walioteuliwa kufanya operesheni hizo. Wakati afisa anayehusika na masuala ya rais safari za rais amesema hizo ni "dhana kwa watu ambao hawana hatia".

Magavana wa Kivu Kaskazini na Ituri, Jenerali Luboya Nkashama na Jenerali Constant Ndima, wanasemekana kuwa na hatia ya unyanyasaji kwa kutumia vyeo vyao vya kutoa amri. "Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, Luteni-Jenerali Ndima aliwaamuru wapiganaji wakundi la waasi la MLC (Movement for the Liberation of Congo) ambapo mnamo mwaka 2002 liliongoza operesheni ya mbaya huko Ituri iliyoitwa " Futa ubao " (Effacer le tableau), anasema Thomas Fessy, mtafiti katika shirika la Human Rights Watch.

"Na kulingana na wachunguzi, yeye mwenyewe alikuwa na jina la utani ambalo kwa kweli lilitoka kwa kitengo maalum cha kundi hilo la waasi, kilichojumuisha wapiganaji kutoka kwa kundi lingine la waasi, RCDN (Rassemblement des Congolais démocrates nationalistes). Kwa upande wake, Luteni-Jenerali Ludoya, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi katika jeshi kwa waasi wa RCD Goma, anaweza kuwa nahatia kupitia cheo chake cha kutoa amri kwa mauaji, ubakaji na unyanyasaji mwingine uliofanywa na vikosi hivi ”, ameendelea mtafiti huyo.

Thomas Fessy amebaini kuwa uteuzi huu ni unaonyesha wazi tabia ya kutoadhibu watu visa vya "unyanyasaji vinavyfanywa na makundi ya waasi na vikosi vya jeshi.