DRC

Machafuko yazuka baada ya kufutwa kazi kwa Zoe Kabila kama gavana wa Tanganyika

Zoé Kabila hapa ilikuwa mwezi Februari 2012 huko Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu)
Zoé Kabila hapa ilikuwa mwezi Februari 2012 huko Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu) Junior D. Kannah / AFP

Zoé Kabila Mwanzambala, gavana aliyeondolewa mamlakani katika mkoa wa Tanganyika, amekaribisha hatua ya upigaji kura ya bunge la mkoa kwa kutokuwa na imani naye. Ameomba raia kuwa watulivu. kauli ilio kinyume kabisa na ndugu zake pamoja na anasiasa wenzake wa upinzani

Matangazo ya kibiashara

Makundi ya vijana yalishambulia makazi ya wabunge kutoka Umoja Mtakatifu wa Kitaifa ambao, kulingana na vijana hao, walipiga kura ya kutokuwa na imani na gavana Zoé Kabila Mwanzambala na timu yake. Jaynet Kabila, mbunge wa kitaifa na dada mkubwa wa gavana aliyeondolewa mamlakani, ametoa wito kwa raia kulaani kile wao na wahusika wengine wa kisiasa wanaona kama ukiukaji wa Katiba.

Wito kwa utulivu

Akikasirishwa na ghasia zilizozuka katika mkoa huo, Zoé Kabila amewatolea wito raia kuwa watulivu. Ujumbe aliowasilisha kupitia msemaji wa serikali ya mkoa wa Tanganyika Dieudonné Kamona. Zoé Kabila pia anasubiri mahakama ya DRC itoe uamuzi katika kesi inayohusiana nakutimuliwa kwake mamlakani Alhamisi wakati wa mkutano ambao ulileta pamoja wabunge kumi na tatu tu waliochaguliwa wa Umoja Makatifu wa Kitaifa.

Zoé Kabila anabaini kwamba amefanyiwa madhila hayo kutokana na kukataa kwake kujiunga na muungano Mtakatifu wa Kitaifa uliloanzishwa na Rais Felix Tshisekedi aliyevunja muungano wa FCC / CACH. Uamuzi wa Mahakama ya Katiba unasubiriwa kwa hamu.