CHAD-USALAMA

Baraza la Amani na Usalama la AU kuijadili Chad

Mji mkuu wa Chad, Ndjamena.
Mji mkuu wa Chad, Ndjamena. © David Baché/RFI

 Umoja wa Afrika unaazimia, kuanzia Jumatatu, kujadili suala la uwezekano wa vikwazo dhidi ya utawala wa Chad siku kadhaa baada ya mwanae hayati Kdriss Deby kupewa mamlaka ya uongozi wa nchi.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili hali ilikuwa shwari, baada ya vurugu zilizogubika maandamano iliyofanywa Jumamosi huko Ndjamena na kote nchini na  muungano wa raia wa Wakit Tama.

Wakati huo huo Jeshi la Chad limesema vikosi vyake vimefanikiwa kuwashinda waasi wanaojiita FACT baada ya makabiliano ya mwezi mmoja Kaskazini mwa nchi hiyo.

Makabiliano dhidi ya waasi hao, yalisababisha kifo cha rais wa nchi hiyo Idriss Derby, mwezi uliopita.

Kudhirisha ushindi huo, jeshi la Chad limewaweka hadharani waasi 156 waliokamatwa wakati wa operesheni hiyo.