DRC

DRC: Maswali yaibuka kuhusu uteuzi wa wahalifu wa kivita kwa kuwalinda raia

Wanajeshi wa FARDC wanapita karibu na askari wa MONUSCO huko Mavivi, Kivu Kaskazini (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa FARDC wanapita karibu na askari wa MONUSCO huko Mavivi, Kivu Kaskazini (picha ya kumbukumbu). AFP - ALAIN WANDIMOYI

Wakati huu majimbo ya Ituri ya Kivu Kaskazini yakiwa chini ya uongozi wa kijeshi kwa lengo la kuwatokomeza waasi, maswali yameendelea kuibuka kuhusu hatua ya serikali, kuwateua wanajeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwatesa raia na kukiuka haki za binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Uwepo wa maafisa wa Congo katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini, wanaotafutwa na mahakama ya kijeshi kwa uhalifu mkubwa lakini hawajawahi kufikishwa mahakamani, umeharibu uhusiano kati ya UUmoja wa Mataifa na jeshi la DRC, FARDC, na hivyo kuzuia uungwaji mkono kamili wa operesheni a kijeshi.

Wakati huo huo raia wanawatuhumu kwa kutofanya vya kutosha kumaliza mauaji katika mikoa hiyo.

Tangu Alhamisi, hali ya dharura inatekelezwa vilivyo katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Lengo ni kukomesha mauaji katika mikoa hii miwili. Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch linasema lina wasiwasi kuhusu  watu walioteuliwa kufanya operesheni hizo. Wakati afisa anayehusika na masuala ya rais safari za rais amesema hizo ni "dhana kwa watu ambao hawana hatia".

Magavana wa Kivu Kaskazini na Ituri, Jenerali Luboya Nkashama na Jenerali Constant Ndima, wanasemekana kuwa na hatia ya unyanyasaji kwa kutumia vyeo vyao vya kutoa amri. "Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, Luteni-Jenerali Ndima aliwaamuru wapiganaji wakundi la waasi la MLC (Movement for the Liberation of Congo) ambapo mnamo mwaka 2002 liliongoza operesheni ya mbaya huko Ituri iliyoitwa " Futa ubao " (Effacer le tableau), anasema Thomas Fessy, mtafiti katika shirika la Human Rights Watch.