ETHIOPIA

Ethiopia yadai kuua wapiganaji wengi na kukanusha ripoti mbalimbali za mauaji

Vita vya Tigray vilisababisha uharibifu mkubwa, Machi 18, 2021.
Vita vya Tigray vilisababisha uharibifu mkubwa, Machi 18, 2021. REUTERS - BAZ RATNER

Ethiopia inasema idadi kubwa ya watu waliouawa katika jimbo la Tigray ni wapiganaji wala sio raia kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa.

Matangazo ya kibiashara

Hili limebainishwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Fikadu Tsega, kauli ambayo ni kinyume na ripoti za mashirika ya Kimataifa ikiwemo umoja wa Mataifa.

Jeshi la Ethiopia mwezi Novemba mwaka uliopita, lilivamia Tigray kupambana na vikosi vya TPLF na hatua ambayo imesbabisha mauaji makubwa na maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

Hivi karibuni Serikali ya Ethiopia ilikanusha madai yaliyotokewa na Marekani kwamba, majeshi ya Addis Ababa yamefanya mauaji na maangamizi ya kikaumu katika jimbo la Tigray la kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ethiopia ilisisitiza kuwa, kile kilichoelezwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kwamba, kumefanyika mauaji ya utokomezaji kaumu katika jimbo la Tigray ni uwongo na madai matupu yasiyo na mashiko.