LIBYA-MAREKANI

Marekani yamteua mjumbe maalum kwa Libya kwa mara ya kwanza tangu 2011

Balozi wa Marekani Richard Norland wakati wa mkutano na Marshal Haftar kando ya mkutano wa Berlin huko Ujerumani, Januari 20, 2020 (picha ya kumbukumbu)
Balozi wa Marekani Richard Norland wakati wa mkutano na Marshal Haftar kando ya mkutano wa Berlin huko Ujerumani, Januari 20, 2020 (picha ya kumbukumbu) AFP/LNA War Information Division

Richard Norland atahudumu kama mjumbe mpya maalum wa Marekani nchini Libya wakati akikalia wadhifa wake kama balozi huko Tripoli, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alitangaza Jumatatu katika taarifa iliyowasilishwa na ubalozi wa Maekani.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, balozi huyo ataongeza juhudi za kidiplomasia "kushikilia mchakato wa kisiasa katika mazingira mazuri hadi uchaguzi wa Desemba".

Richard Norland, aliyeteuliwa kuwa balozi mwaka 2019 nchini Libya tayari amekuwa akihudumu kama mjumbe maalum asiye rasmi kwa kuzidisha matamko juu ya mamluki na kufanya ziara nchini Tunisia, Misri, Uturuki na Usiwi  ili kuendelea na faili ya Libya.

Uteuzi wake rasmi unamaanisha kuwa Washington itaongeza "mazungumzo na washirika wake pamoja na raia wa Libya" ili kuandaa uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu, imesema taarifa hiyo.

Kulingana na waangalizi kadhaa, uamuzi huu ni mageuzi ya Marekani kwa faili ya Libya. Wakati wa utawala wa Donald Trump, maafisa wa Mrekani walikuwa wakituma jumbe zinazopingana kwa kambi mbili hasimu: walikuwa wanaunga mkono serikali ya Fayez el-Sarraj na, wakati huo huo, wakimhimiza Marshal Khalifa Haftar kushambulia mji mkuu Tripoli.

Rais Joe Biden anataka kujitofautisha na utawala uliopita, hasa kuhusu Afrika, na analenga ufanisi zaidi katika mzozo huu wa Libya ambao umedumu kwa zaidi ya miaka kumi.