DRC-AFYA

Watu 5 wapatikana na maambukizi ya kirusi kutoka India

Watu wachukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya corona nchini DRC
Watu wachukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya corona nchini DRC © Siegfried Forster / RFI

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetangaza kesi tano ya maambukizi ya Corona kutoka nchini India. Nchi ambayo inaendelea kushuhudia maambukizi zaidi na vifo vingi kutokana na aina hiyo ya kirusi cha Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hili limethibitishwa na Waziri wa Afya nchini humo Jean-Jacques Mbungani Mbanda akiwa jijini Kinshasa. 

Shirika la Afya Duniani WHO linaonya kuwa mataifa ya Afrika huenda yakashuhudia ongezeko la maambukizi ya virusi hivyo kufuatia kuwepo kwa aina mpya ya maabukizi kama ya India.

Wiki iliyopita watafiti walibaini kuwa watu watano walipatikana na maambukizi ya virusi vya COVID-19 aina ya India nchini Kenya.

Maambukizi hayo yalibainika kutoka kwenye sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha mbolea magharibi mwa Kenya.

Nchi hiyo kwa muda imesitisha safari za abiria kwenda India wiki mbili zilizopita.