DRC-AFYA

DRC : Watoto waendelea kukabiliwa na Utapia Mlo Kasai

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto UNICEF nchini humo linasema, kati ya tarehe 14 mwezi Apili na Mei 1, watoto 29 walilazwa hospitali kwa kusumbuliwa na utapiamlo.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto UNICEF nchini humo linasema, kati ya tarehe 14 mwezi Apili na Mei 1, watoto 29 walilazwa hospitali kwa kusumbuliwa na utapiamlo. AFP

Watoto katika jimbo la Kasai nchini Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanakabiliwa na Utapia Mlo kufuatia baa la njaa linalosababishwa na ukosefu wa chakula cha kutosha.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto UNICEF nchini humo linasema, kati ya tarehe 14 mwezi Apili na Mei 1, watoto 29 walilazwa hospitali kwa kusumbuliwa na utapiamlo.

Mwaka 2018 shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto UNICEF lilisema watoto 770 000 katika jimbo la Kasai Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikumbwa na utapia mlo na 400,000 miongoni mwao walikuwa katika hali mbaya, huku likitaka hatua za dharura za kiutu kuchukuliwa. 

Watu Milioni 27.3 wanakabiliwa na baa la njaa nchini DRC kufuatia sabbau mbaliumbali ikiwemo ukosefu wa usalama Masharii mwa nchi hiyo.