CHAD-SIASA

Wakit Tama laitisha maandamano Mei 19, jeshi laonya raia

Wanajeshi wa jeshi la Chad wamesimama kwenye magari kando ya waasi kutoka Front for Change and Concord in Chad (FACT), ambao walikamatwa pamoja na vifaa vyao wakati wa mapigano kaskazini mwa nchi, katika makao makuu ya jeshi huko N'Djamena, Chad Mei 9, 2021
Wanajeshi wa jeshi la Chad wamesimama kwenye magari kando ya waasi kutoka Front for Change and Concord in Chad (FACT), ambao walikamatwa pamoja na vifaa vyao wakati wa mapigano kaskazini mwa nchi, katika makao makuu ya jeshi huko N'Djamena, Chad Mei 9, 2021 REUTERS - Oredje Narcisse

Nchini Chad, vuguvugu la Wakit Tama linalowashirikisha wanaharakati na wanasiasa wa upinzani, limetangaza maandamano mengine tarehe 19 mwezi huu dhidi ya uongozi wa jeshi nchini humo, kushinikiza madaraka kukabidhiwa kwa raia.

Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano yaliyoandaliwa na vuguvugu hilo lakini halikufanikiwa baada ya kuzuiwa na uongozi wa jeshi nchini humo na wanaandamanaji kadhaa kukamatwa.

Hayo yanajiri wakati hivi kaibuni jeshi la Chad lilitangaza kumalizika kwa operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa Front for Alternation and Concord in Chad (FACT).

Wakati huo huo kundi la waasi la FACT limepuuzia kauli hiyo ya jeshi na kusema kuwa litaendelea na mapambano kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.