DRC-USALAMA

DRC : Saba waangamia katika shambulio la waasi wa ADF Ngaka

Huko Ituri, urushianaji wa risasi kati ya wanamgambo na wanajeshi yamesababisha vifo vya watu kumi na mmoja (picha ya kumbukumbu).
Huko Ituri, urushianaji wa risasi kati ya wanamgambo na wanajeshi yamesababisha vifo vya watu kumi na mmoja (picha ya kumbukumbu). MONUSCO/Abel Kavanagh

Watu saba wameuawa katika kijiji cha Ngaka Wilayani Mambasa mkoani Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mkoa ambao kwa sasa unaongozwa na jeshi, baada ya rais wa nchi hiyo kutangaza kuwa mkoa huo na ule wa Kivu Kaskazini uko chini ya uongozi wa jeshi kutokana na kudorora kwa usalama.

Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Uganda wa ADF wananyooshewa kidole kuhusika na mauaji hayo.

Ni mara ya kwanza wilaya ya mambasa mkoani Ituri kushuhudia mfululizo wa mashambulizi ya waasi wanaoshukuwa kuntoka kundi la ADF mwaka huu, kulingana na Idriss Kukodila, mkuu kiongozi wa wilaya ya mambasa. 

Kulikuwa na Shambulizi katika kijiji cha Ngaka, wahuni hao walichoma nyumba kadhaa na kuiba mbuzi na kuku na Kila walicho pendezwa nacho lakini Jeshi linaendelea kuwaska waliotekeleza shambulio hilo", amesema Idriss Kukodila.

  Manusura na mashahidi wanasema wasi hao waliingia na kuzingira vijiji vya Ngaka, Masana, Matonge na Sambango. Mbali na  mauaji ya raia na makumi ya wakazi wa vijiji hivyo kutekwa nyara na kubebwa mstituni, kumeshuhudiwa pia uporaji wa mali ya umma na nyumba kuchomwa moto. 

"Tunachoka na mauaj , wanatuondoa katika nyumba , tumefanya kosa gani!  Tumekosea nini! , tunataka usalama hatutaki vita, raia wa kigeni warejee nchini”

Mai 8 raia wengine 2 waliuawa mjini Lukaya wilayani Mambasa na muasi 1 ku uawa zimeripoti duru za Jeshi la FARDC.