MEDITERANIA

Mvutano waibuka kati ya walinzi wa pwani ya Libya na wavuvi wa Italia

Boti ya uvuvi ya Aliseo ikisindikizwa na Walinzi wa Pwani wa Italia Mei 8, 2021.
Boti ya uvuvi ya Aliseo ikisindikizwa na Walinzi wa Pwani wa Italia Mei 8, 2021. AP - Roberto Rubino

Tangu wiki iliyopita, Italia ilielezea hasira yake dhidi ya Libya. Wavuvi wanaotuhumiwa kukiuka eneo la baharini wanasema walishambuliwa kwa risasi moto na walinzi wa pwani ya Libya.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya hasira ya Italia, balozi wa Libya huko Roma amebaini kwamba tukio hili halitakuwa na athari yoyote kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Siku ya Alhamisi, Mei 6, Italia ilishutumu tabia isiyofaa kikosi cha walinzi wa pwani ya Libya, na kuomba wavuvi wa Italia wasikaribie eneo linaloelezwa kuwa "hatari".

Mlinzi wa pwani wa Libya, kwa upande wao, alijibu tu Jumapili hii, Mei 9, akibainisha kuwa walipiga risasi tu za onyo. Kisha wanalaani "uvamizi haramu" na "ukiukaji unaorudiwa" wa boti za Uvuvi za Italia katika maji ya eneo la Libya.

Tofauti kuhusiana na mpaka kwenye eneo la baharini

Kulingana na meya wa Mazzara huko Sicily, ambapo meli inayohusishwa ilitokea, nahodha wa meli hiyo alipata jeraha la mkono na meli hiyo ina alama za risasi. Boti hiyo ya Italia ilikuwa wakati wa tukio karibu maili thelathini kutoka pwani ya Libya. Sheria ya majini ya Umoja wa Mataifa inafafanua maji ya eneo la kila nchi kwa maili 12 za baharini. Mamlaka ya Libya inafikiria tangu mwaka 2005 kwamba maji katika eneo yanaendelea hadi maili 30.