DRC-USALAMA

DRC: Watu Elfu tano wayatoroka makazi yao kufuatia mapigano Kivu Kusini

Watu zaidi ya Elfu tano hawana makaazi na sasa wanaishi katika kambi ya wakizimbizi ya Ruzizi.
Watu zaidi ya Elfu tano hawana makaazi na sasa wanaishi katika kambi ya wakizimbizi ya Ruzizi. AFP - ALEXIS HUGUET

Maelfu ya watu wameyakimbia makwao kufuatia mapigano kati ya makundi ya waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Matangazo ya kibiashara

Hili limethibitishwa na maafisa wa usalama na waasi, baada ya kuzuka kwa mapigano hayo katika jimbo la Kivu Kusini katika maeneo ya Ziwa Tanganyika katika mpaka wa nchi hiyo na Burundi. 

Makundi ya waasi ya Biloze Bishambuke na  Twigwaneho kutoka kabila la Banyamulenge ndio wanaoripotiwa kukabiliana. 

Aimable Nabulizi, msemaji wa kundi la waasi la Biloze Bishambuke ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa, kundi la waasi la Twigwaneho lilivamia ngome yao. 

Msemaji wa jeshi la FARDC Dieudonne Kasereka, amethibitisha kuendelea kwa mapigano haya ambayo amesema yamekuwa yakiendelea kwa mwezi mmoja sasa. 

Watu zaidi ya Elfu tano hawana makaazi na sasa wanaishi katika kambi ya wakizimbizi ya Ruzizi.