SUDAN-UCHUMI

Sudani kulipa mzigo wa madeni inayodaiwa

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok.
Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok. REUTERS - HANNIBAL HANSCHKE

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amesema ana imani kuwa nchi yake inaweza kulipa deni la kigeni la Dola Blilioni 60 inalodaiwa. 

Matangazo ya kibiashara

Hamdok amesema atatumia mkutano wa kiuchumi kati ya mataifa ya Afrika na Ufaransa mwezi Oktoba kupata mwafaka kuhusu deni hilo. 

Nchi hiyo inadaiwa na Shirika la fedha duniani IMF miongoni mwa mashirika mengine kama Benki ya dunia, wakati huu serikali ya Khartoum ikiahidi kuimarisha uchumi wake.

Mwanzoni mwa mwezi Januaria Serikali ya Sudan ilisaini mkataba wa makubaliano na Wizara ya Hazina ya Marekani ili kuwatolea zaidi ya dola bilioni 1 kila mwaka kulipa deni lake kwa Benki ya Dunia.