NIGER

Ukosefu wa usalama Niger: Wanakijiji wanaokimbia mashambulizi wawasili Tillaberi

Wanajeshi wa Niger wakipiga doria (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa Niger wakipiga doria (picha ya kumbukumbu). ISSOUF SANOGO / AFP

Tangu Alhamisi, Mei 13, katika eneo hilo la mipaka mitatu, maelfu ya wanakijiji kutoka mkoa wa Anzourou wamekuwa wakiwasili katika mji wa Tillaberi kwa makundi. 

Matangazo ya kibiashara

Watu hawa waliokimbia makazi yao wanatafuta kimbilio baada ya kulazimishwa kuondoka katika vijiji vyao na watu wenye silaha ambao pia wameiba ng'ombe zao na kuharibu ghala zao za chakula.

Wakazi kutoka vijiji vya Niger magharibi wamelazimika kutoroka makazi yao kutokana na mashambulio ya wanajihadi. Maelfu wamekuwa wakiwasili katika mji wa Tillaberi kutoka mkoa wa Anzourou kutafuta kimbilio.

"Hawa ni watu ambao walilazimika kutembea kilomita nane, au hata kilomita ishirini na tano, kabla ya kufikia njia kuu ambapo wanaweza kupata magari ya kuwaleta hapa Tillaberi," amesema Adamou Oumarou, mwanaharakati wa haki za binadamu na mwanachama wa shirikamoja la kiraia la Tillaberi .

Anzourou, iliyo na vijiji 24, ni sehemu ya mkoa mkubwa na thabiti wa Tillaberi, iliona ukubwa wa zaidi ya 100,000 km2 na iko katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu" kati ya Niger, Mali na Burkina Faso.