AFRIKA KUSINI-HAKI

Afrika Kusini: Kesi ya Jacob Zuma yaahirishwa hadi Mei 26

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Jacob Zuma ni pamoja na udaganganyifu na uhujumu uchumi kuhusu ununuzi wa silaha hizo.
Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Jacob Zuma ni pamoja na udaganganyifu na uhujumu uchumi kuhusu ununuzi wa silaha hizo. ROGAN WARD POOL/AFP

Kesi ya ufisadi inayomkabili rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, imeahirishwa mpaka tarehe 26 mwezi huu, ambapo anatarajiwa kukubali au kukataa mashtaka dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Zuma ambaye aliongoza nchi ya Afrika Kusini kama rais wa nne, kati ya mwaka 2009 mpaka kujiuzulu kwake mwaka 2018, anatarajiwa kukataa mashtaka dhidi yake.

Kabla ya mahakama kutoa uamuzi huu, wafuasi wake walikusanyika nje ya mahakama katika mji wa Pietermaritzburg kabla ya Zuma mwenyewe kujitokeza.

Rais huyo wa zamani anakabiliwa na makosa 16 ya ufisadi, kuhusu mkataba wa ununuzi wa silaha wenye mabiloni ya Dola kati ya serikali ya Afrika Kusini na kampuni ya Ufaransa, Thales, kwa lengo la kuboresha ulinzi wa nchi hiyo miaka ya tisini.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili ni pamoja na udaganganyifu na uhujumu uchumi kuhusu ununuzi wa silaha hizo.

Mashahidi 217 wanatarajiwa kutoa ushahidi dhidi ya rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini