SUDAN-UCHUMI

Ufaransa kuipatia Sudan mkopo wa dola bilioni 1.5 kuisaidia kulipa IMF

Waziri wa Uchumi wa Ufaransa, Bruno Le Maire mbele yta Bunge la Ulaya, Oktob 23, 2018.
Waziri wa Uchumi wa Ufaransa, Bruno Le Maire mbele yta Bunge la Ulaya, Oktob 23, 2018. FREDERICK FLORIN / AFP

Ufaransa itasaidia Sudan, ambayo inakabiliwa na mzigo mkubwa wa deni, kulipa deni lake inalodaiwa na shirika la Fedha la kimataifa, IMF,  kwa kuikopesha dola Bilioni 1.5, Waziri wa Uchumi wa Ufaransa Bruno Le Maire ametangaza leo Jumatatu, Mei 17.

Matangazo ya kibiashara

Ufaransa itafanya kazi "kuiondolea Sudan mzigo wa deni lake haraka iwezekanavyo", amesema Bruno Le Maire, kabla ya Mkutano wa Kimataifa unaolenga kuunga mkono kipindi cha mpito nchini Sudan. Mkutano ambao umeanza tangu saa 7:00 mchana katika mji mkuu wa Ufaransa, siku moja kabla ya mkutano wa kimataifa juu ya kufufua uchumi barani Afrika.

Rais Emmanuel Macron atathibitisha ahadi hii ya kifedha kutoka Ufaransa katika hafla hii, amesema waziri huyo, ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa kibiashara kati ya Ufaransa na Sudan ulioandaliwa na shirika la waajiri la Ufaransa MEDEF, ambao Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah amehudhuria.

Wawakilishi kutoka IMF, Umoja wa Afrika, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na hata Benki ya Dunia watakuwapo leo mchana pamoja na wanasiasa kupata suluhisho la haraka kuhusu mzigo huo wa deni, ambalo ni karibu dola Bilioni 50. Lengo lililotajwa ni kuiunganisha tena Sudan katika nyanja za kimataifa za ufadhili.

Kwa upande wake, Benki ya Maendeleo ya Afrika inapanga tena kuangalia upya deni la Sudan linalokaribia kufikia kiasi cha dola milioni 430 na ufadhili wa ziada. Inabidi kuonyesha msaada wetu maalum benki hiyo imebaini.