DRC-USALAMA

DRC: imamu wa pili auawa Beni katika kipindi cha mwezi mmoja

Moja ya barabara za mji wa Beni, Desemba 20, 2018.
Moja ya barabara za mji wa Beni, Desemba 20, 2018. AFP - ALEXIS HUGUET

Licha ya kuanza kutumika kwa hali ya dharura kwa wiki mbili katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, imamu mwingine anayepinga vikali msimamo mkali wa kidini aliuawa katika eneo la Beni Jumanne tarehe 18 Mei.

Matangazo ya kibiashara

Djamal Moussa, ambaye pia ni kiongozi wa shirika la kiraia katika mji wa Mavivi, aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake. Ni imamu wa pili kuuawa katika mwezi huu wa Mei katika eneo la Beni peke yake.

Kulingana na Donat Kibwana, mkuu wa wilaya ya Beni, Djamal Moussa aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake na mtu asiyejulikana baada ya kutoka kudiriki swala ya  jioni.

Muuaji alimlenga kichwani kabla ya kutimkia msituni. Karibu kilomita kumi kutoka jiji la Beni, huko Mavivi, imamu huypo alikuwa ni mwenye ushawishi na alikuwa ni mtu anayesikilizwa katika jamii yake ndogo.

Alionya mara kadhaa waandishi wa habari na mamlaka juu ya harakati na dhuluma zinazofanywa na kundi wa waasi wa Uganda wa ADF katika eneo hilo.

Sheikh Ali Amini aliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa swala ya Magharibi, huyo alikuwa imam wa kwanza kuuawa katika eneo la Beni mwezi huu wa Mei.

Kiongozi huyo alikuwa akikemea vitendo vya wanamgambo wa kiislamu kwenye eneo hilo, shirika la habari la Reuters liliripoti