CHAD

Chad: Umoja wa Afrika wataka kipindi cha mpito kutamatika katika miezi 18

Makao makuu ya Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, Februari 5, 2020.
Makao makuu ya Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, Februari 5, 2020. Paulina Zidi/RFI

Umoja wa Afrika (AU) umeitaka mamlaka iliyochukua madaraka nchini Chad baada ya kifo cha rais Idriss Déby Itno ikamilishe "katika miezi 18" mchakato wa "mpito wa kidemokrasia" utaowezesha uchaguzi "huru, wa haki na wa kuaminika".

Matangazo ya kibiashara

Katika azimio lililotolewa Alhamisi kwenye wavuti yake, Baraza la Amani na Usalama la AU (PSC) "linasisitiza haja kamilikwa kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kidemokrasia kukamilika katika tarehe ya mwisho ya miezi 18 iliyotangazwa na Baraza la kijeshi la Mpito, CMT, Aprili 20, 2021" .

Baraza la Amani na Usalama la AU (PSC) linataka tarehe hiyo ya mwisho iheshimishwe, likibaini kwamba hakutakuwa na hoja yoyote ya kuongeza muda wa kipindi cha mpito na wala hilo halitokubalika kwa AU".

PSC pia inataka na serikali ya raia kugawana madaraka, na kwamba viongozi wa kijeshi wanaoshikilia madaraka kutoshiriki katika uchaguzi.