DRC-USALAMA

Ituri: Jeshi ladai kudhibiti vijiji zaidi ya 20 kutoka mikononi mwa waasi Djugu

Jeshi la DRC, FARDC,  linaendelea na mashambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo CODECO katika mkoa wa Ituri.
Jeshi la DRC, FARDC, linaendelea na mashambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo CODECO katika mkoa wa Ituri. Photo MONUSCO/Abel Kavanagh

Wiki mbili baada ya kuzinduliwa kwa operesheni za kijeshi katika eneo la Djugu, mkoani Ituri, nmashariki mwa DRC, jeshi limesema limedhibiti zaidi ya maeneo ishirini, yaliyokuwa yamekaliwa na wanamgambo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kutoka Ituri, vijiji vilivyoondolewa mikononi mwa wanamgambo wa CODECO hasa, ni vile vilivyo katika sekta za Walendu Pitsi, Djatsi na Tatsi.

Kudhibitiwa kwa maeneo haya kumewezesha kurejea makawo kwa "baadhi ya wakaazi" ambao walitoroka eneo hilo kufuatia ukosefu wa usalama.

Hata hivyo baadhi ya wakazi ambao walikimbilia msituni wakati wa mapigano kati ya makundi ya waasi na vikoi vya serikali bado wanasita kurudi katika vijiji vyao.

Kulingana na mashirika ya kiraia katika eneo la Djugu, watu hawa wanahofia kuwa "watachukuliwa kama wanamgambo wa CODECO" na vikosi vya usalama.

Lakini Luteni Jules Ngongo, msemaji wa jeshi huko Ituri, akinukuliwa na Redio OKAPi inayodhaminia na Umoja wa Mataifa nchini DRC, amewahakikishia usalama wao. "FARDC wapo" kwa ajili ya usalama wa raia wote wa DRC ", amesema.

Luteni Jules Ngongo, hata hivyo, ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kujitenga na wanamgambo na kushirikiana na jeshi ili eneo la Djugu lipate amani ya kudumu.