LIBYA

Libya: Wasiwasi watanda juu ya uchaguzi ujao wa mwezi Desemba 2021

Bunge bado halijapiga kura ya bajeti ya Waziri Mkuu wa Libya Abdel Hamid Dbeibah (kwenye picha), inayochukuliwa kuwa ya juu zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Bunge bado halijapiga kura ya bajeti ya Waziri Mkuu wa Libya Abdel Hamid Dbeibah (kwenye picha), inayochukuliwa kuwa ya juu zaidi katika historia ya nchi hiyo. © Mahmud Turkia, AFP

Nchini Libya, hali ya kutoelewana imeongezeka wakati ikikaribia tarehe ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 24.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano ya kisiasa yaliyopatikana hivi karibuni kupitia mkutano uliowashirikisha wadau wote, waliokutana chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa, unalenga kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi huo katika kuendeleza mchakato wa amani na utulivu.

Hali ya kuoelewana imejitokeza katika masuala ya Katiba na sheria ihusuo uchaguzi huo. Baadhi wanataka kufanyike kura ya maoni juu ya Katiba muda unakwenda. Kuhusu kuunganishwa tena kwa taasisi huru, bado hali ni tete.

Mchakato wa kisiasa nchini Libya unaingia katika hatua ngumu. Uchaguzi wa mwezi Desemba 2021 unaonekana kuingiliwa na hitilafu mbalimbali. Mkutano wa pili wa Berlin utaandaliwa Juni 23 ili kuweka mambo sawa nchini. Mkutano huo utatanguliwa na mikutano miwili muhimu iliyopangwa huko Tunis na Morocco wiki ijayo.