DRC-HAKI

DRC: Kesi ya mauaji ya Yumbi yafikishwa mbele ya mahakama

Nyumba iliyochomwa moto huko Yumbi nchini DRC.
Nyumba iliyochomwa moto huko Yumbi nchini DRC. RFI/Patient LIGODI

Mapigano ya kikabila kati ya Batende na Banunu mwishoni mwa mwaka 2018 katika mkoa wa Mai Ndombe yalisababisha vifo vya watu wengi na makumi ya maelfu ya wakimbizi wakimbilia nchi jirani ya Congo-Brazzaville.

Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizo pia zilisababisha kufutwa kwa uchaguzi wa urais na wabunge katika sehemu hiyo ya nchi.

Kulingana na mashirika ya haki za binadamu, makabiliano hayo yalikuwa yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 500. Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa ulikuwa ulikadiria watu zaidi ya 800 kuwa ndio walipoteza maisha katika makabiliano hayo. Zaidi ya watu 17,000 walikimbilia nchi jirani ya Congo-Brazzaville, na leo, kulingana na vyanzo vyetu, bado kuna wakimbizi 11,000 upande wa pili wa Mto Kongo.

Jumanne hii, mbele ya Mahakama Kuu ya jeshi huko Kinshasa, washtakiwa 62, wanaozuiliwa katika gereza la jeshi la Ndolo, watasikilizwa katika kesi hiyo. Walikamatwa katika eneo la Yumbi, na kupelekwa mjini Kinshasa.