MALI-SIASA

Mali: makamu wa rais awaweka kando viongozi wa mpito

Rais wa mpito wa Mali Bah N'Daw na makamu wa rais Assimi Goïta.
Rais wa mpito wa Mali Bah N'Daw na makamu wa rais Assimi Goïta. © AFP/ Michele CATTANI

Ni vigumu kujuwa kwa sasa hatima ya Rais wa Mali Bah N’Daw na Waziri wake Mkuu Moctar Ouane. Waawili hao walichukuliwa Jumatatu hii, Mei 24, 2021 na kupelekwa kwenye kambi ya Kati, karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako, na wanajeshi walio karibu na kamati ya kitaifa ya wokovu wa watu, iliyohusika na mapinduzi ya Agosti 18, 2020.

Matangazo ya kibiashara

Kanali Assimi Goïta, makamu wa rais wa mpito, na mtu mwenye ushawishi mkubwa katika Baraza la Kijeshi la Mpito (CNSP) ametoa taarifa kwenye runinga ambapo ametangaza "kuwaweka kando ya mamlaka yao" wawili hao.

Kanali Assimi Goïta, kionozi wa mapinduzi na makamu wa rais wa mpito, anaishutumu serikali ya Moctar Ouane kwa kupoteza imani ya washirika kuhusika na mgomo naoendelea sasa.

Zaidi ya yote, anamkosoa Waziri Mkuu kwa kuweka pamoja orodha ya serikali yake mpya, "kwa makubaliano na rais wa mpito" lakini "bila kushauriana na makamu wa rais", akimaanisha yeye mwenyewe. Na kukumbusha kuwa, kulingana na hati ya mpito, yeye ambaye ndiye anayesimamia ulinzi na usalama wa nchi. Kanali Sadio Camara na Modibo Koné, walioondolewa mamlakani siku moja kabla ya kutangazwa serikali mpya, hawatajwi, lakini nafasi zao mbili, Ulinzi na Usalama, zimetajwa hapa.

Maswali mengi yasiyo na majibu

Kanali na Makamu wa Rais Assimi Goïta kwa hivyo anahakikisha kwamba alilazimika "kumuweka kando" rais na waziri mkuu. Je! hapa mtu anaweza kuelewa kuwa wametimuliwa madarakani au wanazuiliwa kwa muda mfupi? Je! Kanali Assimi Goïta ndiyekiongozi kwa sasa wa Mali? Je! Kiongozi mpya wa nchi na kiongozi mpya wa Serikali watateuliwa? Haya yote ni maswali muhimu ambayo mazungumzo ya sasa yatalazimika kujibu. Ikumbukwe kwamba jamii ya kimataifa hadi sasa imeepuka kutumia neno "mapinduzi" na inapendelea kutumia neno "kulazimishwa" ili kutoa nafasi nzuri kwa mazungumzo.