MALI-SIASA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuijadili Mali

Assimi Goita, rais wa Baraza la Kitaifa la Wokovu la Watu (CNSP) nchini Mali, wakati wa mkutano wa ECOWAS huko Accra, Septemba 15, 2020.
Assimi Goita, rais wa Baraza la Kitaifa la Wokovu la Watu (CNSP) nchini Mali, wakati wa mkutano wa ECOWAS huko Accra, Septemba 15, 2020. © Nipah Dennis / AFP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura siku ya Jumatano kujadili hali nchini Mali, baada ya jeshi kuchukua tena uongozi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Matangazo ya kibiashara

Kanali Assimi Goita ambaye pia ni Makamu wa rais aliagiza kukamatwa kwa rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu  Moctar Ouane na kufuta serikali ya mpito baada ya kuwashtumu viongozi hao wawili kwa kutomshirikisha kuhusu mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Hayo yanajiri wakati mpatanishi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, Goodluck Jonathan, aliwasili jana, Jumanne Mei 25 alasiri, huko Bamako kujaribu kuzuia mgogoro uliosababishwa na mapinduzi mapya yaliyoendeswa na kuli la wanajeshi waliohusika na mapinduzi ya mmwezi Agosti 2020.

Mazungumzo yalilianza jana jioni, huko Bamako, kati ya Goodluck Jonathan na ujumbe wake upande mmoja, na kwa upande mwingine, wawakilishi wa vionozi wa mapinduzi ya zamani.

 Wakati huo huo Rais wa Ufaransa Emmauel Macron amelaani hatua ya jeshi nchini Mali.