AFRIKA KUSINI-HAKI

Rais wa zamani wa Afrika Kusini afutilia mbali mashitaka ya rushwa yanayomkabili

Zuma amesema ni muathiriwa wa kampeni ya kisiasa ya kumchafulia jina inayofanywa na kundi pinzani katika Chama tawala cha ANC (African National Congress).
Zuma amesema ni muathiriwa wa kampeni ya kisiasa ya kumchafulia jina inayofanywa na kundi pinzani katika Chama tawala cha ANC (African National Congress). ROGAN WARD POOL/AFP

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekanusha mashitaka ya rushwa yanayomkabili, ulaghai na utakatishaji fedha kuhusiana na mpango wa ununuzi wa silaha kwa kiasi cha dola bilioni 2 wakati akiwa naibu rais.

Matangazo ya kibiashara

Zuma, anayekabiliwa na uchunguzi mwingine wa ufisadi uliofanywa wakati akiwa rais, anatuhumiwa kwa kukubali dola 34,000 kila mwaka kutoka kwa kampuni ya silaha ya Ufaransa Thales, ili nayo kampuni hiyo ilindwe dhidi ya uchunguzi kuhusiana na biashara hiyo.

Zuma amesema ni muathiriwa wa kampeni ya kisiasa ya kumchafulia jina inayofanywa na kundi pinzani katika Chama tawala cha ANC (African National Congress).

Mawakili wa Zuma wanataka mwendesha mashitaka wa serikali Billy Downer aondolewe kwenye kesi hiyo, kwa misingi kuwa hana mamlaka ya kuongoza kesi hiyo. Upande wa mashitaka umeomba muda zaidi kujibu ombi hilo na uamuzi utafanywa Julai 19.

Hata hivyo Zuma anakabiliwa na mashitaka 18 yanayohusiana na mkataba huo wa 1999.