ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Joe Biden ataka kusitishwa kwa mapigano Tigray

Biden ametaka pande zinazohusika na mzozo huo hasa wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea kuhakikisha kuwa misaada ya kibiandamu inawafikia watu wanaoendelea kuteseka.
Biden ametaka pande zinazohusika na mzozo huo hasa wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea kuhakikisha kuwa misaada ya kibiandamu inawafikia watu wanaoendelea kuteseka. Anna Moneymaker GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP

Rais wa Marekani Joe Biden amelaani kuendelea kushuhudiwa kwa mzozo wa jimbo la Tigray na kutaka visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu kukoma.

Matangazo ya kibiashara

Biden kupitia kwa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya White House, amesema mzozo huo wa mezi sita katika jimbo la Tigray unamsikitisha.

Ameelaani ripoti ya wakaazi wa jimbo la Tigray kudhulumiwa na vikosi vya usalama, ikiwemo visa vya wanawake na wasichana kubakwa, visa ambavyo amesema ni lazima sasa vifike mwisho.

Aidha, Biden ametaka pande zinazohusika na mzozo huo, hasa wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea kuhakikisha kuwa misaada ya kibiandamu inawafikia watu wanaoendelea kuteseka.

Umoja wa Mataifa kupitia mkuu wake anayehusika na misaada ya kibinadamu Marck Lowcock ,umeonya kuwa kuna hatari kubwa ya kutokea kwa ukame katika jimbo hilo na msaada wa haraka unahitajika ndani ya miezi miwili ijayo.

Mzozo wa jimbo la Tigray ulianza mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed  kutuma wanajeshi kukabilkiana na vikosi vya eneo hilo vilivyokuwa vimeshambulia kambi za jeshi la nchi hiyo.