UFARANSA-AFRIKA KUSINI

Emmanuel Macron kujadili COVID-19 Afrika Kusini

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya rais huko Pretoria, Afrika Kusini Mei 28, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya rais huko Pretoria, Afrika Kusini Mei 28, 2021. © RFI/Pierre Firtion

Baada ya Rwanda, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yuko ziarani nchini nchini Afrika Kusini leo Ijumaa. Ziara hii imelenga suala la afya wakati nchi hii ndiyo imeendelea kuathirika zaidi na mgogoro wa COVID katika bara la Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Mara tu alipowasili nchini Afrika Kusini, Emmanuel Macron alipokelewa na mwenzake Cyril Ramaphosa. Ziara hii ya kiserikali ya Emmanuel Macron ni ya kwanza nchini Afrika Kusini. Ziara ambayo ilitarajiwa kufanyika mwaka jana, lakini iliahirishwa kwa sababu ya mgooro wa kiafya.

Ziara hii ina changamoto kadhaa. Afya kwanza, kwa kuwa Afrika Kusini ni nchi barani Afrika ambayo imeendelea kuathirika zaidi na mgogoro wa COVID-19. Programu ya msaada wa uzalishaji wa chanjo kwa Afrika ilitarajiwa kuzinduliwa leo mchana wakati Rais Emmanuel Macron alitarajia kuzuru Chuo Kikuu cha Pretoria. Mpango ulioandaliwa kwa miezi mingi na Ufaransa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Benki ya Dunia.

Kufufua biashara

Ziara hii pia ni muhimu kiuchumi. Biashara kati ya nchi hizo mbili imeathiriwa vibaya na mgogoro wa kiafya. Lengo kwa hivyo ni kufufua uwekezaji wa Ufaransa. Suala la mwisho ni la kidiplomasia. Marais hao wawili watajadili hali ya Msumbiji hasa. "Afrika Kusini ni mshirika mkubwa katika bara la Afrika na kwa upana zaidi, ni mwanachama pekee kutoka Afrika wa nchi zilizostawi kiviwanda (G20) iliyoalikwa mara kwa mara kwenye vikao vya Kundi la mataifa Saba yaliyostawi zaidi kiviwanda (G7)", wasaidizi wa rais wa Ufaransa wamesema.