UFARANSA-USHIRIKIANO

Msimamo mkali wa kidini: Rais wa Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake Mali

Wanajeshi wa Ufaransa kutoka Operesheni Barkhane, katika mkoa wa Menaka (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa Ufaransa kutoka Operesheni Barkhane, katika mkoa wa Menaka (picha ya kumbukumbu). RFI/ Anthony Fouchard

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametishia kuondoa jeshi la Ufaransa ikiwa Mali itaingia katika mfumo wa msimamo mkali wa dini ya Uislamu.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na Gazeti la Jumapili (JDD), rais wa aUfaransa pia amesema anaunga mkono mchakato wa mpito baada ya kile alichokuwa ameelezea kama "mapinduzi yasiyokubalika".

Maneno haya yanakuja wakati viongozi wa Afrika Magharibi wanakutana kutatua swali lenye utata juu ya jibu lao kwa jaribio la pili la mainduzi ya jeshi nchini Mali, lililongozwa na Assimi Goïta.

Onyo la Emmanuel Macron liko wazi: "Sintashirikiana na nchi ambayo hakuna uhalali wa kidemokrasia tena," amesema katika ukurasa wa Gazeti la Jumapili (Journal de Dimanche). Rais wa Ufaransa anadai "kuwa amefikisha ujumbe" kwa wenzake katika ukanda huo. Njia mojawapo ya kuwashinikiza kabla ya mkutano wa ECOWAS uliopangwa kufanyika Jumapili, Mei 30 alasiri.

Jambo lingine thabiti la mahojiano haya, tishio la kuondolewa kwa kikosi cha Barkhane: "Kwa rais wa Mali Bah N'Daw, ambaye alikuwa mkali sana juu ya uhusiano kati ya utawala na wanajihadi, nilisema" msimamo mkali wa kidini nchini Mali na askari wetu huko? Kamwe sintokubali maishani! " Leo kuna hatari ya kuwepo hali hini nchini Mali. Lakini hali ikiwa hivyo, nitaondoa jeshi langu ”. Maneno haya ya Emmanuel Macron yanamaanisha hasa washirika wa siku za usoni wa Assimi Goïta katika kipindi cha mpito.