NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Wanafunzi kadhaa wa shule ya Kiislamu watekwa nyara

Ripoti zinasema watoto 200 ndio waliokuwa katika Shule hiyo ya Kiislamu ya Salihu Tanko, na haijafahamika ni watoto wangapi walitekwa na ni wapi walikopelekewa.
Ripoti zinasema watoto 200 ndio waliokuwa katika Shule hiyo ya Kiislamu ya Salihu Tanko, na haijafahamika ni watoto wangapi walitekwa na ni wapi walikopelekewa. Kola Sulaimon AFP/Archivos

Watu wenye silaha wamewateka watoto, katika shule moja ya Kiislamu katika jimbo la Niger, ikiwa ni mwendelezo wa visa vya kutekwa kwa watoto nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Polisi katika jimbo la Niger Wasiu Abiodun, amesema watekaji hao waliwasili katika shule hiyo iliyo kwenye mji wa Tegina wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kufyatua risasi hewani kabla ya kutekeleza utekaji huo.

Ripoti zinasema watoto 200 ndio waliokuwa katika shule hiyo ya Kiislamu ya Salihu Tanko, na haijafahamika ni watoto wangapi walitekwa na ni wapi walikopelekewa.

Hata hivyo, afisa wa shule hiyo amesema watoto waliotekwa ni zaidi ya 100 lakini waliokuwa wenye umri kati ya miaka minne na 12 wakarudishwa shuleni.

Utekaji huu umekuja siku moja baada ya wanafunzi 14 waliokuwa wametekwa Kaskazini Maghairibi mwa nchi hiyo kuachiwa huru baada ya kuwa mateka kwa siku 40.

Makundi yenye silaya yameendelea kuwahangaisha wakaazi wa Kaskazini Magharibi na eneo la Kati nchini Nigeria kwa kutekeleza utekaji kama huu ikiwa ni pamoja na kuiba mifungo.

Tangu Desemba mwaka 2020 watu wenye silaha wamewateka watoto na wanafunzi 730.