DRC

Tshisekedi akosolewa kwa kuleta mkanganyiko kuhusu mahitaji ya kibinadamu Goma

Rais wa DRC Félix Tshisekedi.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi. AP - Ludovic Marin

Kauli ya rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, kuwa hali mbaya ya mahitaji ya kibinadamu huko Goma  inadhibitiwa, kufuatia changamoto zilitokea kutokana na mlipuko wa Volcano kutoka mlimani Nyiragongo, na kusababisha maelfu ya watu kuyahama makwao kwa tishio la kutokea kwa mlipuko wa pili, imekosolewa na mashirika ya kiraia na yale ya kutoa misaada.

Matangazo ya kibiashara

Watu laki nne wamelazimika kukimbia mji wa Goma kufuatia amri ya viongozi ambapo baadhi wamekimbilia nchini Rwanda, katikamji wa Bukavu na Sake kwenye umbali wa kilometa 25 na Goma. 

Kauli hiyo ya matumaini imepingwa na mashirika ya kiraia na hata yale ya misaada.

Awali, rais Tshisekedi alifafanua kuwa tishio la kutokea tena kwa mlipuko wa pili, halijaondolewa kwa sababu kuna mtiririko wa tope la volcano chini ya ardhi ambapo mlipuko wa Volcano unaweza kutokea wakati wowote mahali popote katika mji waGoma, wakati watu wengi waliohamishwa katika maeneo hayo wakijaribu kurejea makwao.